Condition:
NEW
Description
Hii ni temperature gauge ambayo inakuonesha joto la engine lakini pia inapiga alarm mara tu engine inapoanza kuoverheat. Hivyo kama hutoona joto likipanda kwenye gauge utasikia sauti ya Buzzer. Hii itakufanya uchukue hatua za haraka hivyo kukuepusha na athari za overheat ikiwa ni pamoja na kununua engine cylinder head, Block au vyote kwa pamoja(mswaki). Baadhi ya watu husema gari ndogo zina mechanism ya kujizima ikipata joto. Hiki kitu siyo kweli, Ndio maana gari ikioverheat mara kadhaa cylinder head, Block au vyote kwa pamoja hupinda. Umeshawahi kujiuliza ni kwanini? Sababu ni kwamba every time engine ikioverheat basi cylinder head and/or block hupinda na kuachia nafasi kwenye combustion chambers. Na hapo ndio engine huanza kumisi na mwishowe kuzima kabisa. Engine ikipoa, vilivyopinda vinarudi mahali pake (Elasticity). Hiyo cycle ikifanyika mara kadhaa cylinder head and/or block inapinda jumla (Plasticity). Kuna msururu wa gari nyingi sana ambazo hazina temperature gauge kwenye dashboard. Hasa gari za Toyota, Mfano wa gari hizo ni IST, Wish,Passo, Noah/Noah Voxy, Vitz, FunCargo, Ipsum, Opa, Nadia, Porte, Probox, Ractis, Raum, Rush, Sienta na nyingine nyingi. Hapo nimejaribu tu kutaja zile gari ambazo zimezoeleka. Changamoto moja ni kwamba gari hizi zinakuwa tu na taa ya joto ambayo huwaka gari ikishaoverheat lakini huwezi kujua kama joto linapanda. Hata kama gari yako ina temperature gauge bado unaweza kufunga hii sababu ya kuwepo kwa buzzer na vitu vingine ambavyo sijaviandika. Kimuonekano ni ndogo sana hata mkononi haijai. Naifunga ndani halafu naiunganisha na sensor yake ya joto ambayo ntakuwa nimeifunga kwenye engine. Bei ni Tsh. 50,000/= tu na ufundi humohumo. Nipo Dar Nipigie