Details
Description
**MaishaSafi Aluminium Works** inawatangazia mafundi wenye sifa zilizoainishwa chini kwa ajili ya kuomba kufanya kazi zifuatazo: - Mafundi Wanaotakiwa: Mafundi Wa **Kuchomelea** (2) Na **Aluminium** (2) (Aluminium and Welding Works) **Waombaji wanatakiwa kuwa na sifa za msingi zifuatazo** i. Muombaji awe na uzoefu usiopungua miaka mitano kwenye kazi tajwa hapo juu, au elimu ya ufundi isiyopungua trade test grade iii na uzoefu wa miaka mitatu. ii. Muombaji awe na ujuzi wa kutosha kufanya kazi hizo zilizotajwa na aambatanishe nyaraka za kazi alizokwisha zifanya.(ikiwemo mawasiliano ya alikowahi kufanya kazi) N.B MAFUNDI WALIOKWISHA FANYA KAZI ZINAZOFANANA NA HIZI WATAPEWA KIPAUMBELE iii. Muombaji awe na wadhamini wawili, namba ya simu ya muombaji na Namba za simu za wadhamini au Barua Kutoka serikali za mitaa. iv. Muombaji Awe Mtanzania Na Aambatanishe Utambulisho Wake ( Kivuli Cha Kitambulisho Cha Uraia(NIDA) Au Mpiga Kura Au Leseni Ya Udereva) Maombi yatumwe kwa email, au piga simu Mwisho wa kupokea maombi ni Mei 31 , 2022