Description
Rafiki-SDO ni shirika lisilo la kiserikali ambalo limekuwa likifanya kazi Tanzania Bara tangu mwaka 2005 likilenga kuboresha upatikanaji wa huduma rafiki za afya ya uzazi kwa vijana walio ndani na nje ya shule, wanajamii na makundi maalum. Rafiki-SDO pia inafanya kazi Kukuza ulinzi wa mtoto, ushiriki wa mtoto katika masuala yanayoathiri maisha yao, uimarishaji wa uchumi kwa jamii, na uhamasishaji wa mabadiliko ya tabia kwa jamii. Pia, Rafiki-SDO inawezesha elimu ya stadi za malezi chanya, kuzuia maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kupitia uhamasishaji upimaji VVU rufaa ya upimaji VVU na kuunganishwa na huduma zikiwemo afya na ustawi wa jamii. Shirika la Rafiki-SDO linatekeleza mradi ACHIEVE kwa kushirikiana na shirika la PACT katika Halmashauri ya wilaya ya Rorya, Bunda na Manispaa ya Musoma. Kupitia mradi huu Shirika la Rafiki-SDO kwa kushirikiana na shirika la PACT limepanga kutoa ufadhili wa Sare za Shule kwa wanafunzi 482 wa shule za Msingi kutoka kaya zenye mazingira magumu. Lengo la ufadhili huu ni kuongeza Morali ya wanafunzi lengwa kuhudhuria shule, kujifunza kikamilifu nakupunguza utoro unaosababishwa na kukosa sare. Shrika la Rafiki-SDO linapenda kuwatangazia fursa watu wote wenye sifa na uwezo; binafsi, Vikundi au Makampuni wanaojishughulisha na kazi za kushona na kusambaza sare za Shule ndani ya mkoa wa Mara kutuma Maombi ya zabuni ili kutimiza lengo hilo la kuwapatia wanafunzi Sare SIFA ZA MWOMBAJI 1. Awe anaendesha shughuli zake katika mkoa wa Mara. Uthibitisho wa hili ni Barua ya utambulisho kutoka Mtendaji wa Kata/Mtaa/kijiji anakofanyia kazi 2. Awe na Uzoefu wa kutosha kukamilisha kazi kwa ubora unaokubalika (Uthibitisho wa kazi sawa na hii kwa siku za nyuma- ambatanisha wasifuwako). 3. Awe na Uwezo wa kukamilisha kazi ya kushona Sare zote kwa muda mfupi usiozidi wiki mbili (uthibitisho wa uwepo wa vifaa na Rasirimali watu wa kutosha kuonyesha idadi ya vyerehani na wafanyakazi ulionao pia ambatanisha mpango kazi wako). 4. Awe anaijua vizuri jiografia ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na Rorya (ufahamu wa shule na aina ya Sare zinazotumiwa) . 5. Awe hajazuiliwa kufanya kazi ya ushonaji na mamlaka yoyote ya kimanunuzi kwa ngazi ya kitaifa au kimataifa. 6. Awe na uhalali wa kufanya biashara kwa kuzingatia sheria na miongozo ya taifa (leseni ya usajili wa biashara husika ambayo haijaisha mda wa kutumika ). MASHARTI MAHUSUSI 1. Uwezo wa kutoa huduma hadi kukamilika bila kuhitaji Malipo ya awali (Malipo yatafayika baada ya kazi kukamilika) 2. Uwezo wa kushona Sare kwa kuuzingatia ubora na vigezo vilivyokubaliwa (kutumia kitambaa, Vishikizo, zipu na nyuzi zenye ubora wa juu) 3. Mhusika ni lazima awe na Risiti ya EFD (risiti ya Mashine) au burua ya Msamaha wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania au Kitambulisho cha Mjasiriamali 4. Awe na uwezo wa kuwasilisha sampuli ya kitambaa kitakachotumika, bei halisi ya kushona na kusambaza Sare kwa walengwa kwa muda uliokubaliwa. 5. Kuzingatia bei halisi ya soko ya kushona, kununua na kusambaza Sare husika kwa walengwa (wanafunzi wa shule za Msingi zilizopo ndani H/mashauri ya wilaya ya Bunda na Rorya) 6. Uwezo wa kukamilisha zoezi la kushona na kukabidhi sare husika kwa walengwa ndani ya siku 14 tangu kusainiwa mkataba. MAANA YA SARE KWA MUJIBU WA TANGAZO HILI Kwa Mujibu wa Tangazo hili Sare za Shule itamaanisha 1. Shati moja kwa kwa wavulana na wasichana. 2. Kaptura moja kwa wavulana . 3. Sketi moja kwa wasichana . 4. Soksi Pea mbili kwa wavulana na wasichana 5. Sweta moja kwa wavulana na wasichana. NAMNA YA KUTUMA MAOMBI Maombi yatumwe yakiwa kwenye bahasha iliyofungwa vizuri kwenda kwa Mkurugenzi mtendaji, Shirika la Rafiki-SDO S.L.P 177, Musoma, pia uwasilishaji wa maombi kwa kukabidhi ofisini inaruhusiwa. MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI Tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ni 26/6/2022 Saa kumi na moja kamili jioni. Tafadhali kumbuka : 1. Rafiki-SDO inahaki ya kufanya marekebisho kwa ajili ya kuboresha taarifa zilizopo kwenye tangazo kwa lengo la kuongeza ushindani. 2. Kuwasilisha maombi ofisini sio kigezo cha muombaji kupewa mkataba wa zabuni husika . 3. Rafiki-SDO itawasiliana na wazabuni watakaokidhi vigezo vya awali kwa ajili ya kuendelea na hatua nyingine zilizopo kwenye mchakato wa manunuzi kwa njia ya zabuni .