07.06.2020Tanzania, Dar Es Salaam

TUNAFANYA CHECK UP KATIKA MIFUMO YA UMEME NA ELECTRONICS KWENYE MAGARI

Negotiable

Description

Je umekuwa ni muhanga wa kununua battery ya gari yako mara kwa mara kwa sababu ya battery ya gari yako kuharibika kila mara? Je umekuwa ni muhanga wa kushindwa kuliwasha gari lako hadi uliboost kwa battery ya gari nyingine? Je baadhi ya mifumo kwenye gari huzima unapokuwa umewasha vifaa vingi vya gari yako? Kama hakuna shida yoyote kwenye gari yako. Battery yako ya gari inatakiwa kudumu kwa miaka 6. Hayo ni baadhi tu ya matatizo ambayo hutokea ikiwa kuna shida kwenye mfumo wa umeme kwenye gari yako. Hayo matatizo yanaweza kuonekana ni madogo lakini yanaweza kukuingiza kwenye gharama kubwa au hata kuyagharimu maisha yako. Baadhi ya matatizo huwa hayaoneshi dalili na hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kufanya check up kwenye mfumo wa gari yako. Hivyo basi nikiwa kama mtaalamu, Ninafanya check up ya mifumo ya umeme kwenye magari kwa gharama nafuu sana. Nitakagua na nitakuonesha shida ipo sehemu gani. Nitakagua Short circuit, Open circuit pamoja na relays. Gharama zangu ni nafuu sana. Na pia kama mtu ana gari ya kawaida kazi inaweza kuchukua nusu saa mpaka saa moja. Ila kama gari yako ni ya kisasa, kazi inaweza kuchukua masaa mawili hadi matatu(Hapa gharama itaongezeka kidogo tofauti na mwenye gari la kawaida). Pia kama kama utahitaji nikufanyie check up ya sensors, switches na components kama sparking plug, coil on plug, sparking plug wires, injector nozzle n.k. ninaweza kukufanyia. Baadhi ya hivi vitu huondolewa kwenye magari kwa madai ya kuwa ni vibovu wakati vingine huwa huwa ni vizima au vingine huhitaji kusafishwa tu na kurudishiwa na vikafanya kazi bila shida. Hivyo watu huingia gharama kubwa ambazo huenda wangeziepuka. Napatikana Dar es salaam (Magomeni, Mwembechai). Pia kama una tatizo kwenye engine au automatic gearbox tuwasiliane. Faida moja ambayo utaipata kwa mimi kukuhudumia ni kupata ushauri wa kitaalamu bure siku nyingine utakapokuwa na tatizo kwenye gari yako(Hasa kwa matatizo yanayohusiana na engine na warning lights za kwenye dashboard. Kwa maelezo zaidi tunaweza kuwasiliana kwa namba ambayo ipo chini ya tangazo hili. Unaweza kupiga, kutuma meseji kawaida au whatsapp. Asanteni.

Autoelectrical E.

Member since 2020.
xxx xxx xxx xxx

User

Location

Dar Es Salaam