26.01.2022Tanzania, Dar Es Salaam

Fundi Umeme Wa Magari DSM

Negotiable

Description

Taa ya Check engine Kwenye gari zipo sababu nyingi zinaweza kuwasha taa ya Check engine, mfano; 1.Kufa kwa sensors na components zingine za umeme/electronics Kukatika kwa wires zinazoenda/kutoka kwenye sensors na components zingine za umeme/electronics Kuvuja kwa hewa (Vacuum leak). Kubadilika kwa taarifa za vifaa ambavyo vipo calibrated. Baadhi ya vitu kufanya kazi chini ya kiwango. Poor electrical contact ambayo mara nyingi husababishwa na uchafu, kutu n.k. Na mengine mengi sana. Hivyo hata suala la urekebishaji wa matatizo haya ya check engine, unatofautiana kulingana na aina ya tatizo na zipo namna nyingi sana za kurekebisha kama kubadili kifaa, kuunga wires, kusafisha, calibration, n.k. Gari inaweza kuwasha taa ya check engine na mtu akaona au asione mabadiliko yoyote kwenye gari lake, mfano taa ya Check engine inaweza ikawaka na ikaja na mabadiliko yafuatayo. Gari kukosa nguvu Engine kumisi(misfire) Kelele kwenye engine Gari kuzima Gari kutetemeka Gari kutoa moshi mwingi Gari kusumbua kuwaka Gari kutumia mafuta mengi Rough Idle (Gari haitumilii sailensa) Kushtuka wakati unaendesha. Zipo nyingi sana. Kwa kifupi kitu chochote kikiharibika kwenye engine hii taa inaweza kuwaka hivyo inakuwa ni ngumu kukisia muda mwingi kwamba hiyo taa imewaka kwanini, ni mpaka pale tutakapofanya computer diagnosis. Pia muda mwingine unaweza kupata hayo matatizo niliyokueleza hapo juu lakini gari yako isiwashe taa yoyote kwenye dashboard. Kwa maana hiyo siyo kila tatizo litawasha taa ya Check engine ndio maana ni muhimu kupima. Kwenye gari nyingi(isipokuwa gari za Toyota), Check engine huwaka endapo kuna tatizo kwenye engine. Gari nyingi za Toyota na gari zote zinazotumia control unit(ECU) moja kwa engine na gearbox check engine inaweza kuwaka kwa sababu ya engine au gearbox. Sisi katika kufanya computer Diagnosis, tunafanya yafuatayo, Tunapima kwanza ili kujua tatizo, (Computer Diagnosis). Hata kama gari haijawasha taa yoyote tunaweza kugundua tatizo kwa kupima. Tunakipima kifaa kilichoonesha kuwa na tatizo Tuna pima wires zinazokuja kwenye hicho kifaa kama zipo sawa pamoja na kuangalia hali ya wires kama zimechoka. Tunakagua maeneo mengine ambayo yanaweza kupelekea hilo tatizo, Tunarekebisha tatizo. Pia katika kupima Kuna majibu ambayo huwa yanakuja moja kwa moja, Ila yapo mengine ambayo huwa yanahitaji muda zaidi. Nimetumia Alama ya Check engine kama mfano lakini taratibu ni zilezile kwa alama zote zilizopo kwenye dashboard. Hivyo ikiwaka taa yoyote tunaweza kuwasiliana. Ikiwa unahitaji huduma yoyote kwenye gari lako kati ya hizi nilizozitaja hapa chini basi tuwasiliane FULL SYSTEMS DIAGNOSIS AND LIVE DATA ANALYSIS (GHARAMA NI TSH. 50,000/= TU KWA BRAND YOYOTE YA GARI. HII INAANGALIA MIFUMO YOTE YA GARI LAKO KAMA KUNA SHIDA PAMOJA NA UFANISI WA SENSORS NA VITU VINGINE MBALIMBALI. ENGINE DIAGNOSIS AND LIVE DATA ANALYSIS KWA BRAND YOYOTE YA GARI. GHARAMA NI TSH. 30,000/=. HII INAANGALIA MIFUMO YOTE KATIKA ENGINE YA GARI LAKO KAMA KUNA SHIDA PAMOJA NA UFANISI WA SENSORS NA VITU VINGINE MBALIMBALI. KUREKEBISHA MATATIZO KAMA GARI KUKOSA NGUVU, ENGINE KUMISI, KUWASHA TAA YA CHECK ENGINE, MATATIZO YA AUTOMATIC GEARBOX N.K. USHAURI TUWASILIANE,

Benjamin Peterson

Member since 2022.
xxx xxx xxx xxx

User

Location

Dar Es Salaam