Details
Description
Kwa niaba ya mteja wetu wenye Bar, Restaurant & Lounge tunahitaji meneja wa Vyakala na Vinywaji kujaza nafasi iliyo wazi kwa sasa. Maelezo: Kusimamia biashara ya Bar, Mgahawa & Lounge kwa ujumla wake. Kuhakikisha kuna mawasilianao mazuri na wauzaji wa vinywaji, Kuweka oda kwa wakati, kuhuisha mikataba na watoa wanaoleta huduma kama nyama au vinywaji na kusimamia malengo ya biashara. Kuajiri na kufundisha wahudumu jinsi ya kutoa huduma bora. Wajibu na Majukumu: • Kufanya kazi kwa karibu na wasimamizi wa zamu ya mchana na usiku kuhakikisha mafunzo yanaeleweka na huduma zinatolewa katika ubora sahihi. • Kuhakikisha kiwango cha huduma kinachotolewa kinazingatia lengo la kampuni • Kuhakikisha ufanisi unaongezeka • Kusimamia nidhamu ya watendaji wote waliopo chini ya idara hii • Kusimamia matengenezo ya miundo mbinu wezeshi kama vyoo, masinki na viti • Kundika taarifa ya kazi ya kila siku • Kusimamia usalama wa wanywaji na kutoa usaidizi ukihitajika muda wote • Kuhakikisha wateja wanaridhika kwa kiwango kikubwa • Kujibu malalamiko ya wateja ipasavyo na kwa umakini • Kuongeza ubunifu wa huduma mara kwa mara • Kupima utendaji wa wahudumu na kushauri maeneo ya kuimarisha mara kwa mara • Kusimamia Usafi wa mazingira na Vifaa vyote vya huduma • Kujenga picha nzuri ya huduma yetu kila wakati • Kusimamia Gharama za uendeshaji • Kutengeneza mkakati wa mauzo Vigenzo • Elimu ya shughuli za hotel na ukarimu kwa ujumla kwa kiwango cha kuanzia cheti/Astashahhada • Uzoefu angalau miaka 4 ya kufanya kazi kama Msimamizi wa Chakula na vinywaji katika Bar, Restaurant au Lounge za kisasa katika miji mikubwa Tanzania • Kiongozi imara, mwenye hamasa, na ujuzi mkubwa wa kushughhhulika na wafanyakazi wa Bar na wateja • Ujuzi mzuri wa kusimamia fedha kwenye mazingira yenye wateja zaidi ya 3000 kwa usiku mmoja • Uwezo wa kufanya kazi usiku mpaka asubuhi • Uaminifu na nia ya kukuwa katika shughuli za namna hii • Mtu mwenye uwezo wa kujisimamia mwenyewe kwa kiwango kikubwa