Description
Damu nyekundu huambata na mambo haya; 1. Maambukizi Baadhi ya maambukizi kama vile, pangusa na kisonono, yanaweza kusababisha kupata hedhi mara 2 kwa mwezi. Kama ukiona damu kabla hujaanza kipindi chako cha hedhi, basi jitahidi kufika hospitali haraka bila kuchelewa. 2. Ujauzito Kutokwa na damu yenye rangi yoyote wakati wa ujauzito yaweza kuwa ishara au isiwe ishara. Wakati mwingine, hata hivyo huwa ni dalili za mimba kutoka. NUKUU: Wakati mwingine wanawake hutokwa na damu wakiwa wajawazito na baadaye huja kujifungua watoto wenye afya. Kila tatizo liko tofauti. Ni vyema kufika hospitali mapema ikiwa kama unaona damu wakati wa ujauizto. 3. Uvimbe Wa Fibroid Uvimbe huu wa fibroid ndani ya tumbo la uzazi unaweza kusababisha kutokwa na damu nyingi sana wakati wa hedhi au mwaka mwingine wakati wa mzunguko wa hedhi. Unaweza kuwa uvimbe mkubwa au mdogo na hivyo kusababisha dalili zingine kama vile maumivu na presha au tumbo kujaa gesi. Je, Damu Ya Hedhi Yenye Rangi Ya Waridi(Pink) Humaanisha Nini? Damu yako inaweza kuwa na muonekano wa rangi ya waridi hapo mwanzo au mwishoni mwa kipindi chako cha hedhi, hasa kama unatokwa na matone ya damu. NUKUU: Damu hii nyepesi inaweza kuonyesha dalili kwamba damu imechanganyikana na uteute wako wa shingo ya kizazi, na hivyo kuifanya rangi kufifia. Rangi ya waridi huambatana na mambo haya yafuatayo; 1. Homoni Ya Estrogen Kushuka Wakati mwingine damu ya hedhi yenye rangi ya waridi inaweza kuashiria kiwango kidogo cha homoni ya estrogen mwilini mwako. Homoni ya estrogen husaidia kuimarisha ukuta wa tumbo la uzazi. Pasipokuwepo homoni hizi, unaweza kutokwa na damu wakati mwingine katika mzunguko wako wote, huku ikipelekea kuona matone ya damu yenye rangi tofautitofauti, hasa ya waridi. Baadhi ya visababishi vya kiwango kidogo cha homoni ya estrogen ikiwa ni utumiaji wa madawa ya mpango wa uzazi yasiyokuwa na estrogen 2. Kupata hedhi Katikati Ya Mzunguko Wa Hedhi Unaweza ukaona rangi hii karibu na kipingi cha mpevuko wa yai.Tena, pale damu inapotoka kwenye tumbo la uzazi huchanganyikana na ute ute msafi wa shingo ya kizazi, inaweza kuonekana kuwa yenye rangi nyekundu yenye kufifia au ya waridi. 3. Mimba Kuharibika Ikiwa kama una ujauzito, uteute wenye rangi ya waridi unaotoka ukeni unaweza kuwa kiashirio cha mimba kuharibika. Dalili zingine huwa ni tumbo kuuma, kuchomachoma, kutokwa na vinyamanyama ukeni, na dali za mimba kutoka. Karibu kwa shwali ushauri pendekezo matibabu.