Description
FAHAMU KUHUSU U.T.I NA FANGASI SUGU. U.T.I na fangasi ni tatizo kubwa ambalo huwapata wanawake wengi duniani mara kwa mara. Husababishwa na bakteria anaitwa E. coli ambaye huwa wanaishi kwenye utumbo mnene sehemu za tundu la haja kubwa, mwanamke anaambukizwa kirahisi sababu anapokuwa anachuchumaa kwenye haja kubwa au ndogo. Madhara yake kwenye kibofu cha mkojo baada ya kuwa wengi wanahamia mwenye figo, ndio maana leo hii wanawake wengi wanaumwa figo. Figo zao zimeharibika sababu ya U.T.I. na kufa kifo cha ghafla. Tafiti zinaonyeshwa kuwa nchini marekani watu milioni nane (8.1m) hupata U.T.I kila mwaka. MIWASHO. Kawaida mwanamke ana ulinzi ukeni kwake, yaani bakteria wazuri wanaishi kule kwa ajili ya kulinda uke, japo pia bakteria wabaya wanaishi kule lakini kwa uwiano, ya kwamba wale wazuri wanakuwa wengi ,kuliko wabaya . Sasa ikitokea kwamba wale bacteria wabaya wakawa wengi, hapo ndio utaona miwasho kwa mwanawake haishi kujikuna mara kwa mara. FANGASI. Inasababishwa na jamii ya fungi anaitwa CANDIDA. Seli za fangasi na bacteria wazuri huishi ukeni bila tatizo lolote.Tatizo linakuja endapo ukuaji wa fangasi hawa ukeni watakuwa wengi kushinda wazuri. Basi hapo ndio inapotokea ugonjwa wa fangas na miwasho mingi. DALILI ZA U.T.I 1. Kukojoa mara kwa mara. 2. Mkojo kuwa na harufu kali. 3. Kusikia kichefu chefu na kupatika. 4. Maumivu ya misuli na tumbo hasa chini ya kitovu. 5. Kusikia maumivu wakati wa kukojoa. 6. Maumivu ya kiuno. 7. Kuwashwa sehemu za siri. 8. Kuhisi maumivu wakati wa kujamiiana. 9. Kupata vidonda vya ukeni. 10. Kuvimba na kuwa mwekundu kwa mdomo wa inje wa uke. 11. Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri baada ya tendo la ndoa. 12. Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au kijivu unaoweza kuwa mwepesi au mzito au majimaji. VISABABISHI VYA FANGASI. 1. Mabadiliko ya homoni katika kipindi cha upevushwaji wa mayai kwa mwanamke kipindi cha ujauzito, utumiwaji wa uzazi, wa mpango na kukoma kwa hedhi. 2. Upungifu wa kinga mwilini: Mtu mwenye upungufu wa kinga mwilini kama vile mwenye kuugua kansa, ukimwi, magonjwa mbalimbali yenye kupunguza kinga ya mwili. 3. Kukosa usingizi stress, vidonda sehemu za siri,matumizi ya antibiotics, kuweka marashi sehemu za siri. 4. Watu wanaougua kisukari ambao hawawezi kudhibiti kwa kutumia dawa za kisukari, inakuwa kwenye damu na hicho kisukari ndiyo chakula kikuu cha hao fangasi. Hata wanawake ambao wanapenda kula vyakula vya sukari nyingi kama vile chocolates, soda, na vingine vyenye sukari nyingi ambavyo ni chakula cha fangasi. 5. Mazingira ya joto hii inamaanisha nguo ambazo tunatakiwa kuvaa kama vile chupi za cotton hasa kwa wanawake, hazihitaji joto sababu bacteria wabaya wanakuwa wengi sana na kusababisha miwasho na FANGAS 6. Kondomu na mbegu za kiume huharibu hali ya asidi iliyopo ukeni ambayo ni ya muhimu sana maana inasaidia kukinga uke usiingiliwe na bacteria wabaya. MADHARA MAKUBWA YA FANGASI NA U.T.I. Kupatwa kwa ugonjwa wa Pelvic Inflammatory Disease (PID) maambukizi katika via za uzazi na kupelekea kuwa ngumba, ndio maana wanawake wengi ni wagumba. NAMNA YA KUJILINDA NA U.T.I NA FANGASI. 1. Tumia viini lishe na virutubisho i.e food supplements. 2. Kunywa maji mengi angalau glasi nane kwa siku. 3. Epuka matumizi ya pombe na kahawa. 4. Kunywa maji kabla ya kufanya mapenzi na kojoa baada ya kufanya mapenzi. 5. Jitawaze kuanzia mbele kwenda nyuma. (Front to Back) 6. Kata makucha marefu kwa sababu unavyokwenda chooni kujitawaza huwa