Description
FURSA YA ZAO LA MDALASINI Karibu Nehemia One Pvt Co Ltd. wataalamu wenye uzoefu wa masoko na uzalishaji wa mazao ya kilimo. Tunapenda kukukaribisha kwenye fursa ya uzalishaji wa MDALASINI tunazalisha miche ya mdalasini na kuhamasisha watu kupanda zao hili kwasababu tunafahamu soko lake jinsi lilivo kubwa na linazidi kukua Kwa kasi. Ni zao lenye matumizi mengi hasa kama kiungo kwenye Aina mbalimbali za vyakula. Jambo jema ni kuwa soko lake ni kubwa mnoo katika nchi zote duniani lakini uzalishaji wake ni mdogo mno! MASOKO NA UHITAJI Kwa mujibu wa taaasisi ya utafiti ya persistance market research, thamani ya soko la MDALASINI duniani itafikia Dola za kimarekani bilioni 1.15 mwaka 2030. Matumizi kwenye viwanda vya dawa na vipodozi, viwanda vya chakula ndio ambayo yanafanya uhitaji wake kua mkubwa. Yako makampuni mengi kama IVS na mengine mengi ambayo yanahitaji mdalasini kutoka Tanzania Kwa bei kubwa kwenda nchi za falme za kiarabu, ulaya, na America lakini upatikanaji wake ni wa chini. Uhitaji kwenye soko la kimataifa unaongezeka Kwa kasi kwasababu ya matumizi yake kama kiungo cha chakula, dawa chenye antioxidants, ant inflammatory properties, also helping in heart and stroke, blood sugar, diabetes etc. Kampuni yetu yenye muunganiko na makampuni zaidi ya 60 kutoka nchi mbalimbali duniani huwa inapokea oda nyingi za magome ya mdalasini zaidi ya tani 20 Hadi 500 mara Kwa mara lakini tunakosa mdalasini wa kutosha kutimiza oda hizo. SOKO LAKE KWA TANZANIA Mdalasini unaozalishwa Tanzania haukidhi kabisa mahitaji ambapo ni kiasi cha asilimia 20 Hadi 28 ya uhitaji hivyo kufanya asilimia kubwa ya mdalasini kuagizwa kutoka nchi za bara la Asia kama India, Vietnam, Malaysia na China. Baadhi ya wawekezaji kwenye viwanda vya chakula wameonesha nia ya kujenga viwanda Vya kuchakata zao hili lakini ukosefu wa MDALASINI wa kutosha imekua kikwazo. Licha ya viwanda. Kuna makampuni zaidi ya 100 ambayo yanahitaji zao hili ili kusafirisha kwenda nchi za ulaya, America lakini wanakosa kwasababu ya uzalishaji ni mdogo mnoo!. Aina ya miche ya mdalasini inayooteshwa na kampuni ni (Cinnamomum verum) picha ziko mwishoni baada ya maelezo. UZALISHAJI NA MAENEO YANAYOFAA KWA KILIMO HIKI ✓Mdalasini ni jamii ya mti ambao hukua Kwa urefu wa kuanzia Mita 8 Hadi 15 kutegemeana na eneo mmea ulipooteshwa. ✓Hupendelea eneo la wazi kwenye kiasi cha wastani cha jua. ✓huoteshwa kwenye udongo wenye rutuba ya asili na maji ya wastani. Eneo lenye maji mengi au lenye asili ya kutuamisha maji halifai Kwa uzalishaji wa MDALASINI. ✓uhudumiaji na usafi wa shamba ni muhimu angalau mara moja Kwa mwaka. Ukataji (coppicing) wakati wa kuvuna husaidia machipuo mengi kutokeza. ✓zao hili halihitaji mbolea wala dawa katika ukanda wa kitropiki kama Tanzania ✓udongo wa tifutifu, kichanga -tifutifu wenye wastani wa unyevu nyevu unafaa saana, Na maeneo yenye wastani wa mvua wa mm 2000 mpaka mm 2600 Kwa mwaka. Hustawi kwenye mwinuko kuanzia Mita 10 Hadi 1500 kutoka usawa wa bahari na joto kiasi cha wastani wa digrii 27 za sentigredi ✓mmea hustawi au unaweza kustawi kwenye mikoa ya Morogoro, tanga, pwani, mtwara, Lindi, rukwa, tabora, rukwa, tabora, Kagera, mara, (maeneo yanayo zunguka ziwa Viktoria) mbeya, katavi, kigoma na Zanzibar. ✓ umbali Kati ya mti na mti hutegemea sababu kadhaa 1. Kama shamba lako unazalisha pamoja na mazao mengine kama tangawizi, kahawa, n.k. unatakiwa kuacha nafasi ya mita 4 hadi 5 ili kuipa nafasi Mimea mingine. 2. Kama unapanda Mdalasini peke ake inatakiwa kupanda karibu karibu. Lengo la kupanda karibu ni kuilazimisha miti ikue Kwa kurefuka kupanda juu ili kutafuta mwanga wa jua hivyo utapata shina refu litakalo toa magome mengi. Ukipanda mbali mbali itasababisha miti kuto kukua kupanda juu kwasababu umeipa nafasi ya kutosha kukuza matawi ya pembeni na mwanga wa kutosha. Hii husababisha shina kuwa fupi na kupata magome machache. 3. Umbali Kati ya miti hutegemea pia rutuba ya udongo, muinuko, n.k. VIPIMO VYA UMBALI (1*1), (2*2), (3*3), (1.5*1.5)Mita Kipimo Bora ni (2*2). Kwa kipimo hiki, ekari moja itapandwa miti (30*30=900). MAVUNO 1. Mdalasini huanza kuvunwa kuanzia umri wa miaka miwili. Jambo zuri ni kuwa, baada ya kuvuna, mmea unachipua tena na huvunwa Kwa mwendelezo Kwa kila baada ya miaka miwili Hadi mitatu mpaka baada ya miaka 30 Hadi 45 2. Majani, na mbegu hutumika kuzalisha mafuta ambayo Yana thamani kubwa. Magome hutumika kutengeneza viungo vya chakula, dawa na hata vipodozi. 3.jinsi mmea unavo kaa shambani miaka mingi ndivo ambavyo thamani yake inapanda kutokana na uwingi wa magome yatakayo patikana, kuongezeka Kwa ladha na harufu nzuri ya magome. 4. Kama ikiwekezwa Kwa miaka kuanzia 8 hutoa mapato makubwa Sana kama ifuatavyo . Mti mmoja hutoa kilo kati ya 40 na 50 za magome yaliyo komaa na kukaushwa, majani kiasi cha kilo 200 ambayo pia unaweza kuvuna kila mwaka baada ya mwaka wa tatu tangu kupanda, pamoja na mbegu zake. Kwa idadi ya miti 900 Kwa ekari, kiasi cha magome ni kilo 36000 5. Bei Kwa kilo moja ya magome ya mdalasini ni shilingi za kitanzania 8000 Hadi 8500/kg (bei ya wanunuzi wa ndani) bei huwa ni 9000 Hadi 9500/kg Kwa wanunuzi kutoka nje ya nchi ambao ni wengi na wa uhakika. 6. Makadirio ya mapato ghafi Kwa ekari ni (36000*8000) =288,000,000. Gharama za miche ni shs 2600 Kwa kila mche ambayo huuzwa Kwa oda. Tunatoa huduma bure (Kwa wateja wa miche) Kwa msaada wa namna ya kuotesha shambani, kuhudumia, kuvuna na MASOKO ambayo yanasuburi Kwa hamu kubwa.