image

21.01.2021Tanzania, Tabora

TIBA YA BAWASILI

TZS 175 000

Description

Bawasiri Ni Ugonjwa Gani? ?Mada yetu ya leo itazungumzia tatizo linalowapata watu wengi , wake kwa waume, kwenye sehemu zao za kutolea haja kubwa. Iwapo utapata maumivu kwenye eneo la haja kubwa, ukiona damu au pengine utaona vijinyama vinaning’inia, yaweza kuwa tayari ni mhanga wa tatizo tunalolichambua hivi leo. Mara nyingi dalili hizi hazileti usumbufu mkubwa na huondoka zenyewe bila tiba. Endapo tiba itahitajika, huweza kutolewa na kulimaliza tatizo. Kwa kiswahili, tatizo hili huitwa bawasiri. ? Bawasiri ni uvimbe unaoota ndani na/au kuzunguka tundu la kutolea haja kubwa. ?Awali ya yote, tutaona bawasiri ni nini, kisha tutajadili aina zake, sababu ya uwepo wake na mwisho kabisa, tiba ambazo zinaweza kutolewa kuondoa tatizo hilo. ?Sehemu ya mwisho ya utumbo mkubwa iitwayo anal canal ina urefu wa kiasi cha sentimeta 4 hivi. Sehemu ya chini kabisa ya anal canal ni tundu la kutolea kinyesi nje ya mwili (mkundu). Sehemu ya juu yake inaungana na rectum ambayo pia ni sehemu ya utumbo mpana. ?Kuna mtandao wa veni ndogo (mishipa ya damu) kwenye ngozi inayofunika anal canal. Mara nyingine veni hizi hupanuka na kuruhusu damu nyingi na kuzifanya zitune. Veni hizi zilizotuna na tishu zinazozizunguka zinaweza kutegeneza uvimbe kwenye eneo moja au zaidi, na hii ndiyo huitwa bawasiri, kwa kiingereza piles au pathological hemorrhoids . ?Kuna Aina Ngapi Za Bawasiri? 1️⃣Bawasiri za ndani (Internal piles ) ni zile zinazotokea kwenye eneo la ndani lililo zaidi ya sentimenta 2-3 kutoka kwenye tundu la kutolea kinyesi – kwenye eneo la juu la anal canal. Bawasiri za ndani kwa kawaida hazina maumivu kwa sababu sehemu ya juu ya anal canal haina nyuzi za neva za maumivu. 2️⃣Bawasiri za nje (Exteranl piles) ni zile zinazotokea kwenye eneo lililo chini yake, eneo la chini la anal canal. Bawasiri za nje zaweza kuwa na maumivu kwa sababu eneo la chini la anal canal lina uwingi wa nyuzi za neva za maumivu. ?Watu wengine huwa na bawasiri za ndani na bawasiri za nje kwa wakati mmoja. ?Bawasiri za ndani hupangwa kwa grade, grade 1 hadi 4 kulingana na madhara na ukubwa wake: 1️⃣Grade 1: Ni uvimbe mdogo kwenye ngozi inayotanda anal canal kwa ndani. Ni uvimbe ambao hauonekani au huwezi kuugusa kutokea nje. Bawasiri za aina hii huwapata watu wengi. Bawasiri hizi huweza kukua na kuingia kundi la pili – Grade 2. 2️⃣Grade 2: Bawasiri hizi ni kubwa zaidi. Huweza kujitokeza na kuchungulia nje ya tundu la haja kubwa wakati ukijisaidia lakini hurudi ndani mara moja baadaye. 3️⃣ Grade 3: Ni bawasiri zinazoning’inia nje ya tundu la haja kubwa wakati ukielekea msalani. Unaweza kuvisikia kama vinjinyama kimoja au zaidi vinavyoning’inia nje ya tundu. Ni vijinyama ambavyo unaweza kuvisukumizia ndani kwa kidole. 4️⃣Grade 4: Ni vijinyama ambavyo huning’inia wakati wote nje ya tundu la haja kubwa na huwezi kuvisukumizia kwa ndani kwa kidole. Mara nyingine vinaweza kuwa vibonge vikubwa vya damu Na Dr Daniel....

Daniel D.

Member since 2019.
xxx xxx xxx xxx

User

Location