Quantcast
English
Post your ad

Kupatana News

Nafasi za Uwakala (Agents needed) mkoa wa Arusha

29/01/2020

Kupatana.com, mtandao wa matangazo ya bidhaa mbalimbali zinazouzwa hapa Tanzania. Kupatana.com inatembelewa na idadi kubwa ya watu wanaotafuta bidhaa pamoja na wanaouza bidhaa kila mwezi. Katika kuhakikisha huduma zetu zinawafikia wafanyabiashara na wauzaji mbalimbali kila kona ya Tanzania, sasa tunatoa fursa kwa vijana kuweza kujiingizia kipato cha ziada na endelevu.

                                                     

Fursa hii inakuwezesha kuingiza kipato kwa kuuza nafasi za matangazo katika platforms za Kupatana (desktop website, mobile website, Android app na IOS app) ukiwa kama wakala wa Kupatana. Wakala wa Kupatana atapewa namba maalum  ili kuweza kujitambulisha kwa wateja wake. Vilevile wakala atapatiwa mafunzo maalum ili kumwezesha kufanya kazi zake kwa ufanisi.

 

Hii ni nafasi adimu na ya kipekee kwa mtu yeyote anayehitaji kutengeneza kipato endelevu. Wakala ana fursa ya kuingiza kati ya asilimia 10 hadi 30 ya mauzo yake ya kila mwezi. Unachotakiwa kuwa nacho ni TIN number kutoka TRA pamoja na simu janja (smartphone) yenye bundle la internet. 

 

Tunahitaji mawakala wasiozidi hamsini (50) kwa mkoa wa Arusha. Iwapo wewe ni kijana mchakarikaji na utapenda kuitumia fursa hii, tafadhali wasiliana nasi kwa namba 0769-448-446 / 0683 609 778

 

Tembelea tovuti yetu leo www.kupatana.com #biasharanikupatana